Tuesday, November 8, 2016

 BREAKING NEWS


Kiongozi mstaafu waserikali mwingine Afariki dunia
Huyu ni JOSEPH MUNGAI ambaye kwa taarifa za awali amepoteza maisha leo jion tareh 8 decembar 2016 katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa
P . K . A    JOSEPH MUNGAI  
chanzo TBC 


Anayemkataa Magufuli anawakumbatia mafisadi
Na Adelinus Banenwa 

“Siku za mwizi ni arobaini” haya ni maneno ya wahenga ambayo hayana  kipingamizi kwa hali ya sasa inayoendelea nchini Tanzania baada ya siku takribani therathini na tano tangu tumpate raisi mpya wa awamu ya tano ambaye aliapishwa November 5 mwaka huu na kukabidhiwa nchi kutoka kwa mtangulizi wake
Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli anaendelea kuonekana wa tofauti kutokana na kasi yake ya utendaji japo walio wengi hawashtushwi na kasi yake hiyo kutokana na kujulikana vyema hata wakati akiwa waziri katika wizara mbalimbali kama vile wizara ya ardhi, uvuvi, pamoja na na wizara ya ujenzi
Anajulikana kuwa mtu mwenye misimamo isiyo teteleka, anaichukia rushwa, hana makundi kwenye chama chake, hawakumbatii mafisadi, haya yote yanamfanya aendelee kuwa maarufu na kuzidi kupendwa na watanzania waliokata taama na nchi yao kwa muda mrefu
Katika kampeini zake tangu alipoteuliwa na Chama Cha Mapinduzi CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya uraisi alikuja na kauli mbiu inayosema “hapa kazi tu” wengi wa wananchi walisema kauli hii inaakisi utendaji wake wa kazi  katika chakato wa kuomba lidhaa kwa wananchi wamchague ili awe rais wa awamu ya tano aliweza kutembea kwa barabara zaidi ya kirometa elfu arobaini huku akisisitiza kuwa mabadiriko yanawezekana ndani ya CCM
Uchaguzi uliyokuwa na ushindani usiyo  kuwa wa kawaida na ambao haukuwai kutokea katika historia ya Tanzania tangu ilidhie mfumo wa vyama vingi 1992 na uchaguzi wa kwanza mwaka 1995kwa kuwa hadi siku ya kupiga kura hakujulikana nani atashinda licha ya kuwa “mwamba ngoma uvutia kwake” pengine kutokana na umaarufu wa wagombea hasa kutoka vyama vikuu nchini Chama Cha Mapinduzi CCM kikiwakirishwa na Magufuli na  Chama cha Demokrasia na Maendelea CHADEMA kikiwakilishwa na Edward Lowassa
Tarehe 29 october mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Tanzania jaji mstaafu Damiani Lubuva alimtangaza mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM John Magufuli kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa asilimia 58.46% na kuaapishwa tarehe 5 november  kwa kutekeleza kauli yake ya hapa kazi tu rais Magufuli alianza kazi siku ya pili yake baada ya kuapishwa yaani tarehe 6 kwa kufanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha na kukuta takribani wafanyakazi sita hawapo ofisini wakati ni muda wa kazi
Magufuli hakuishia hapo alifanya ziara nyingine ya kushtukiza  hospitari ya rufaa ya Muhimbili na kukuta hali mbaya kwa wagonjwa pamoja na vifaa tiba huku mashine city scan zikiwa  hazifanyi kazi kwa zaidi ya mwezi mmoja.  maamuzi  ya kuvunja bodi ya muimbili na kumsimamisha kazi mkurugenzi wa hospitali hiyo ilikuwa hatua ya mwanzo katika kuhakikisha utekelezaji wa kauli mbiu yake na kutoa wiki mbili mashine hizo ziwe zinafanya kazi
Ziara za kushtukiza kwa kiongozi huyo hazikuishia hapo,baada ya hapo aliamia bandari na kuibua wizi uliokuwa ukiendelea bandarini hapo ikiwa ni pamoja na upotevu wa makontena, ukwepaji wa kulipa kodi uliokuwa ukifanywa na wafanywa na biashara wakubwa jambo lilimpelekea Rais kumsimamisha kazi mkurugenzi wa  bandari kabla ya kuvunja bodi ya bandari hiyona kulitaka jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa wote kwa ajili ya uchunguzi.
Hatua ya kupunguza matumizi ya serikali na kuelekeza nguvu zake katika kuinua uchumi wa taifa Rais Magufuli ameamua kufutilia mbali baadhi ya sherehe zilizokuwa zimezoeleka kuadhimishwa kwa shamra shamra ndermo na vifijo kama sikukuu ya uhuru , siku ya ukimwi na badala yake fedha hizo zitumike katika kununulia madawa pamoja na vitanda vya hospitali ya rufaa ya Muhimbili na kupanga siku hizo kufanyika usafi wa mazingira nchi nzima “hatuwezi kuadhimisha miaka 54 ya uhuru huku watu wanakufa kwa kipindupindu” alisema Rais Magufuli
Mpaka sasa Rais Magufuli anaendesha nchi akiwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia kasi yake ya utendaji imeonekana kuwa sambamba na Magufuli mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika shirika la reli Tanzania na Zambia (TAZARA) na kugundua madudu ya ubadhirifu wa fedha uliokuwa ukiendelea katika shirika hilo
“Anayemkataa Magufuli anawakumbatia mafisadi” alisema kiongozi wa chama cha ACT Wazarendo Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama hicho alitoa kauli hiyo mnamo November 22 mwaka huu huku akiwataka wananchi kumuunga mkono katika kupambana na ufisadi uliokithiri hapa nchini hasa katika sekta za umma
“Nilipokuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge nilikuwa nikitoa taarifa mbalimbali zinazohusu wizi na uporaji uliofanywa katika ubinafsishwaji, sasa tumepata Rais anayetaka kupambana na ufisadi na kurudisha viwanda hivyo tunapaswa kumuunga mkono”alisema Zitto
Rais Magufuli amevunja rekodi ya watangulizi wake kwa kuendesha nchi zaidi ya siku 30 bila kuwa na baraza la Mawaziri ambapo anafanya kazi na Waziri mkuu pamoja na Makatibu wakuu wa wizara  husika huku utendaji ukionekana kuwa wa kasi ya ajabu licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa zikiwemo za kuwamaliza mafisadi na wala rushwa katika ofisi zote za umma na kudhibiti mianya waliokuwa wakitumia.
Kama alivyofanikiwa kudhibiti safari za nje kwa viongozi na kuzuia viongozi hao kutotumia viti vya daraja la kwanza ndani ya ndege,na kuzuia manunuzi ya magari mapya ya serikali kwa lengo la kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza pato la Taifa.
Utendaji kazi wa Magufuli umesababisha mgogoro mkubwa wa Afrika Mashariki ambapo wananchi kutoka Kenya wamemtaka Rais wao Uhuru Kenyata aige mfano wa Rais wa Tanzania katika kuibua na kudhibiti ufisadi uliokithiri nchini Kenya, vivyo hivyo hata nchini Uganda.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mapema wiki hii ametakiwa na wananchi wake kuiga mfano wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi na kudhibiti rushwa pamoja na mfumuko wa bei nchini Nigeria wakati wakizungumza na shirika la utangazaji BBC
Kauli ya Zitto kuwa anayemkataa Magufuli anawakumbatia mafisadi haina kipingamizi kwani mambo yaliyoshindikana kwa miaka mingi yameweza kufanikishwa ndani ya muda mfupi, ni vyema wananchi wakampa ushirikiano katika safari hii aliyoianzisha



Suleiman Bungara

Mbunge wa kilwa kusini SULEIMAN BUNGARA   (Bwege)

Samsung yavamiwa kwa uchunguzi wa ufisadi wa kisiasa

  • Saa 4 zilizopita
ofisi ya Samsung 
Rais Park ameomba msamaha kwa uhusiano wa karibu na Bi Choi lakini anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu.
Waendesha mashtaka nchini Korea kusini wamevamia ofisi za kampuni ya kielektoniki ya Samsung kama sehemu ya uchunguzi wa sakata ya kisiasa inayomuhusu rais Park Geun-hye.
Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Samsung ilimpatia pesa mtoto wa kike wa Choi Soon-sil, ambaye ni rafiki wa karibu wa rais.
Bi Choi anashutumiwa kutumia urafiki wao kuingilia kati siasa na utoaji wa zabuni za kibiashara.
Samsung imeithibitishia BBC kuwa uvamizi huo ulifanyika ikisema "hakuna maelezo zaidi ".
Rais Park ameomba msamaha kwa uhusiano wa karibu na Bi Choi lakini anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu.
  Bi Choi Soon-sil
Bi Choi Soon-sil alikamatwa tarehe 3 Novemba na kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Katika sakata ya hivi karibuni ambayo imeikumba Korea kusini katika wiki za hivi karibuni , waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Samsung huenda ilitoa dola $3.1m kwa kampuni inayomilikiwa Bi Choi na mtoto wake wakike kwa ajili ya kulipia mafunzo ya mwanae wa kike ya kuendesha farasi mwanae nchini Ujerumani.
Waendesha mashtaka pia wanaripotiwa kujvamia ofisi ya korea kusini ya shirikisho la wamiliki wa farasi na pia ofisi za jumuiya ya masuala ya farasi ya Korea
 Rais Park wa Korea kusini
Rais Park alisema anajuta kwa ''kuwa na imani ya kupita kiasi ''katika urafiki wake na bi Shoi
Bi Choi alikamatwa tarehe 3 Novemba na kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Kwa muda wa siku tatu zilizopita maelfu kwa maelfu ya raia wa Korea kusini wamekuwa wakiandamana katika mji mkuu , Seoul, kudai kujiuzulu kwa rais Park kutokana na sakata hiyo ya ufisadi.
Bi Park alikuwa rais wa kwanza mwanamke wakati alipochaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali mwezi Disemba 2012.

Duterte: Hatununui tena bunduki kutoka Marekani

Rais Duterte
 
Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, amesema kuwa ameagiza kufutiliwa mbali kandarasi ya kununua maelfu ya bunduki kutoka Marekani.
Bw Duterte amesema kuwa taifa lake litatafuta njia mbadala ya kununua silaha hizo kwingine kwa bei nafuu.
Idara ya polisi ya Ufilipino ilikuwa imepangiwa kununua takriban bunduki 26,000 kutoka Marekani.
Uhusiano baina ya nchi hizo mbili ambazo zilikuwa washirika kwa muda mrefu, umedorora tangu Bw Duterte aingie madarakani.
Kumekuwepo taarifa kwamba Marekani ilikuwa tayari imepanga kutoiuzia Ufilipino silaha hizo, kutokana na wasiwasi kuhusu ukatili wa Bw Duterte hasa katika kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya.
Watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa mihadarati wamekuwa wakipigwa risasi na kuuawa.

Matokeo ya uchaguzi yanasubiriwa kwa hamu kubwa

Wamarekani leo wanapiga kura kumchagua atakayerithi kiti cha Rais Barack Obama huku kukiwa na ushindani mkali kati ya wagombea wawili, Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican.
Uchaguzi wa leo unafanyika baada ya wagombea wote wawili kukamilisha kampeni zao katika majimbo muhimu. Katika kampeni yake ya Pittsburgh, Clinton amewataka wapiga kura kukumbatia kile alichokiita matumaini na kuwaleta watu pamoja, kusikilizana na kuheshimiana.
Clinton ambaye amekamilisha kampeni yake usiku wa manene huko North Carolina amesema, ''kuna vitu kadhaa nataka muelewe, kwanza sio suala la jina langu na mpinzani wangu kwenye sanduku la kura, ni aina ya nchi tunayoitaka kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu. Nitafanya kazi kwa moyo wangu wote kama rais kuyafanya maisha yawe rahisi kwa ajili yenu na familia zenu. Hivyo usiku huu naomba kura yako, tuweke historia kwa pamoja,'' mwisho wa kunukuu.
Clinton ambaye ameziita kampeni za mpinzani wake kama zilizoleta mgawanyiko, ameahidi iwapo atashinda kuwa rais wa Marekani, ataiunganisha tena nchi hiyo ambayo imegawika kutokana na kampeni mbaya kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Marekani.
Uchaguzi wenye ushindani mkali
Kwa upande wake Trump akiwahutubia wafuasi wake huko Raleigh, North Carolina, ametaka kuungwa mkono katika vita vyake vya kupambana na mfumo wa ufisadi. ''Uchaguzi huu utaamua kama tunatawaliwa na kundi la wanasiasa mafisadi au tunatawaliwa na watu na kwamba mfumo wa kisiasa ulioshindwa haujaleta chochote bali umasikini, matatizo na hasara,'' alisema Trump.
USA Wahlkampf um Präsidentschaft Kombi Anhänger Clinton / Trump (picture-alliance/AP Photo/R. D. Franklin/ G. Herbert) Wafuasi wa Clinton na Trump
Trump aliendelea kulikosoa Shirika la Upelelezi la Marekani-FBI, baada ya mkuregenzi wake James Comey, siku ya Jumapili kusema kuwa Clinton hawezi kushtakiwa kutokana na kutumia anuani binafsi ya barua pepe wakati akiwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.
Karibu kura za mapema milioni 24 zimepigwa kuzunguka Marekani wakati Comey alipotangaza hapo awali kwamba ataanzisha upya uchunguzi wa kashfa mpya ya barua pepe dhidi ya Clinton. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la Associated Press, idadi hiyo inawajumuisha zaidi ya nusu ya kiasi ya watu milioni 42.5 ambao wamepiga kura zao hadi jana Jumatatu mchana.
Naye, Rais Obama amewasihi Wamarekani kuweka historia kwa kumchagua Hillary Clinton ili aweze kumrithi na kuwa mwanamke wa kwanza kuiongoza Marekani. Akizungumza katika kampeni iliyofanyika Ann Arbor, Michigan, Obama amewasihi wapiga kura wampe Hillary heshima kama waliyompa yeye.
Clinton amemalizia kampeni zake kwenye majimbo muhimu ya North Carolina, Pennsylvania na Michigan, huku Trump akielekea kwenye majimbo ya Florida, North Carolina, Pennsylvania, New Hampshire na Michigan.
Takwimu za mwisho kabisa zinaonyesha kuwa Clinton anaongoza kwa ushindi mwembamba dhidi ya Trump. Utafiti wa maoni uliotolewa na kituo cha Televisheni cha ABC na Jarida la Washington Post umeonyesha asilimia 47 ya wapiga kura 1,763 wanamuunga mkono Clinton, huku asilimia 43 wakimuunga mkono Trump.
Matokeo ya uchaguzi huo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na yanatarajiwa kuanza kutangazwa hapo kesho.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/AP, AFP, Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu

Utajiri wa binti wa rais wa Angola

Isabel Dos Santos ni binti wa kwanza wa Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola na anamiliki utajiri wa kiasi dola bilioni 3.2 za Kimarekani, unaomfanya kuwa ndiye mwanamke tajiri kabisa barani Afrika.
Angola Isabel dos Santos spricht zu Journalisten (Reuters/E. Cropley) Angola Isabel dos Santos binti wa kwanza wa rais wa Angola mwenye utajiri mkubwa barani Afrika
Binti huyo amejijengea himaya yake kwa mapana na marefu na hasa katika mji mkuu Luanda ambao ni miongoni mwa miji ya kifakhari na ghali kabisa duniani.Unapotembea katika mji mkuu wa Angola, Luanda, ni vigumu sana kushindwa kuitambua au kukumbana na alau kampuni moja ya Isabel Dos Santos. Binti huyo wa kwanza wa Rais Eduardo Dos Santos na ambaye ni mwanamke tajiri kabisa barani humo amejenga himaya yake ya utajiri katika moja ya miji ghali kabisa duniani -kutoka sekta ya mawasiliano, benki, televisheni ya setelaiti hadi kwenye spoti - kote huko anamiliki biashara kubwa zenye majina mjini Luanda.
Isabel anahodhi kampuni ya Unitel, ambayo ni kampuni kubwa kabisa ya simu za mkononi nchini Angola ikiwa na matawi 81 ndani ya mji huo mkuu pekee na zaidi ya wateja milioni 10 nchi nzima. Anamiliki msururu wa maduka makubwa, huku akiwa pia na hisa katika mabenki ya BIC na BFA sambamba na katika kampuni ya saruji ya Nova Cimangola.
Umiliki wa kampuni kubwa za mafuta
Afrika Angola Candango Supermarkt in Luanda (DW/P. Borralho) Moja kati ya maduka makubwa yanayomilikiwa na Isabel dos Santos
Na kama haitoshi, mwanamama huyo anasimamia kampuni kubwa ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Sonangol pamoja na klabu ya soka ya Petro de Luanda inayofadhiliwa na kampuni yake.
Almuradi, orodha ya utajiri wa Isabel Dos Santos ni ndefu ikijumuisha pia sekta ya afya na uhusiano wake na kliniki kubwa kubwa nchini humo bila ya kuiweka kando sekta ya biashara ya madini, anasema mwanachama wa upinzani, Nelito Ekuikui:
''Tunaweza kuzungumzia pia sekta ya afya na uhusiano wake na kliniki kubwa kubwa za humu nchini bila ya kusahau sekta ya madini. Kampuni hiyo  hazina ushindani. Hilo ni tatizo kubwa kwa nchi kwa sababu ni vigumu sana kwa wafanyabiashara wengine. Endapo tungekuwa na wafanyabiashara  wapya tungekuwa na nafasi nyingi za ajira.''
Taswira ya Isabel kwa Waafrika
Baadhi ya watu wanamuangalia Isabel Dos Santos kama mfano wa wafanyabiashara barani Afrika ambao wametoa nafasi za ajira zinazohitajika kwa kiasi kikubwa, katika taifa ambalo asilimia 24 ya watu hawana kazi, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014. Lakini Nelito Ekuikui haliangalii suala hilo kwa jicho sawa na hilo. Yeye anasema utajiri wa Isabel na biashara zake nchini Angola hazina mpinzani na hilo ni tatizo. Mwanaharakati wa Angola, Benmedoto Jeremias, anasema kwamba kuwa binti wa rais wa nchi kumemrahisishia mwanamama huyo shughuli zake zote ikilinganishwa na wawekezaji wengine, ''Kila kitu anachokimiliki Isabel Dos Santos kimetokana na upendeleo na fursa anazopata kutoka kwa baba yake. Sio mali alizopata kwa juhudi zake''
Kwa upande mwingine, mwandishi habari Rafael Marques ambaye amekuwa akifuatilia mzizi wa utajiri wa Isabel Dos Santos kwa kipindi cha miaka mingi, anasema kwamba baba yake, Jose Eduardo Dos Santos, amekuwa na dhima kubwa katika kumjengea utajiri huo.
Mwandishi huyo wa habari wa Angola aliiambia DW mapema mwaka huu kwamba kila alichokitaka Isabel, baba yake alihakikisha anakipata. Dos Santos alitumia hadi nafasi yake kama rais kumpa mwanamwe huyo majukumu ya kusimamia fedha katika mikataba mikubwa mikubwa ya serikali, ingawa mara nyingi Isabel amekuwa akizipinga tuhuma hizo za kupendelewa.
Na baada ya kuiongoza kampuni kubwa ya nishati ya mafuta ya Sonangol na kufikia hatua hadi ya kuwa mwekezaji mkubwa nchini Ureno, mkoloni wa zamani wa Angola, wapinzani wanahisi hana tena pa kwenda na sasa huenda akageukia kujaribu katika siasa. Mwanaharakati Benedito Jeremias anakubaliana na hilo akisema mrembo huyo wa miaka 43 huenda ikawa hata ana mipango ya kukirithi kiti kinachokaliwa na baba yake.
Mwandishi:Saumu Mwasimba/Guilherme Correia da Silva
Source: DW-English Page
Mhariri: Mohammed Khelef

Operesheni ya kuikomboa miji ya Mosul na Raqqa

Wapiganaji wa Kikurdi wameshambulia mji unaoshikiliwa na IS Kaskazini Mashariki mwa Mosul. Majeshi ya Irak yanapambana dhidi ya vikundi vya Jihad, Operesheni kama hiyo inafanyika pia Syria kuukomboa mji wa Raqqa.
Mapambano dhidi ya kundi la IS yameingia katika wiki ya nne sasa kwenye juhudi zinazoungwa mkono na majeshi ya kimataifa kwa ajili ya kilidhoofisha kabisa kundi la IS katika nchi za Irak na Syria.  Lengo la mapambano hayo ni kuukomboa mji wa Raqqa huko nchini Syria ambao ndio ngome kuu ya wapigananji wanaojiita Dola la Kiislamu IS na mji wa Mosul wa nchini Irak.
Kikosi kinachoungwa mkono na Marekani kinachowajumuisha wapiganaji wa Kikurdi na wa Kiarabu kimesonga mbele na kufikia karibu na mji wa Raqqa.  Kikosi hicho cha Kikurdi kutoka nchini Syria SDF kimetoa taarifa kuwa wapiganaji wake wamefanikiwa kusonga mbele kuelekea kusini mwa mji wa Raqqa ijapokuwa kinakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa ISIS.
Kwingineko wanajeshi wa Irak wameuteka mji wa Hamam al Alil ulio kusini mwa mji wa Mosul baada ya kufanikiwa kuwatimua wapiganaji wa ISIS wakati huo huo mjini Baghdad wapelelezi wanachunguza kaburi la halaiki lililogunduliwa siku moja kabla ya vikosi vya kijeshi vya Irak kuendelea kusonga mbele katika hatua ya kuukaribia mji wa Mosul.
Miji ya Raqqa na Mosul ndio miji  mikubwa ya mwisho katika nchi za Syria na Irak ambayo bado inashikiliwa na makundi ya wapiganaji wa Jihad na kukombolewa kwa miji hiyo kutalidhoofisha zaidi kundi la wapiganaji wa IS  waliyoiteka tangu mwaka 2014.
Kundi la ISIS taabani
Majeshi washirika  yanayoongozwa na Marekani yalianzisha mapambano dhidi ya IS tangu miaka miwili iliyopita yanaendelea kutoa ushirikiano kwa kutumia ndege za kivita pamoja na vikosi maalum vya kutoa ushauri kuhusu mashambulio ya nchi kavu.
Msemaji wa kikosi cha Kikurdi kinachoungwa mkono na Marekani bibi Jihan Sheikh Ahmed ameeleza kwamba vikosi vya muungano wa wapiganaji wa Kikurdi na Kiarabu vimesonga mbele kilomita 10 katika eneo la kusini kuelekea miji ya Ain Issa na Suluk na kwamba wapiganaji wake wako takriban kilomita 30 kuweza kuufikia  mji wa Raqqa. kwa mujibu wa bibi Ahmed wapiganani wa SDF wameviteka vijiji 10 hadi kufikia sasa na mapambano yanaendelea kama yalivyopangwa.
Syrien PK SDF Strum auf Rakka (Getty Images/AFP/D. Souleiman) Kikosi cha wanajeshi wa SDF
Hata hivyo kamanda wa SDFameeleza kuwa wapiganaji wa kundi la ISIS wanaendeleza mbinu yao ya kuwatumia wapiganaji wa kujitoa muhanga ambao wanatumia magari yaliyojazwa mabomu dhidi ya wapiganaji wa kikosi chake chenye takriban askari 30,000. Maafisa wa SDF wamesema kuwa mapambano hayo huenda yakachukua muda mrefu.
Hatua ya kulizingira kundi la IS kutoka pande zote ndio inayoaminiwa kuwa itafaulu kulimaliza kundi hilo, takriban wataalamu wa kijeshi 50 wa Marekani wanahusika katika operesheni ya kuukomboa mji wa Raqqa huko nchini Syria na wanahusika zaidi katika kutoa ushauri.
Makundi ya kutoa misaada ya kibinadamu yametahadharishajuu ya hatari ya kutumiwa raia na kundim la IS kama ngao au ukuta wa kujikinga katika miji ya Raqqa na Mosul.  takriban watu 34,000 wamepoteza makao yao katika mji wa Mosul tangu operesheni dhidi ya kundi la ISIS ilipoanza tarehe 17 mwezi Oktoba.
Mji wa Mosul una takriban watu millioni moja huku mji wa Raqqa ukiwa na watu 240,000 ambapo inaaminiwa huenda watu elfu 80 wamekimbilia katika mji huo kutoka katika miji mingine ya nchini Syria.
Mwandishi:  Zainab Aziz/AFPE/RTRE
Mhariri: Daniel Gakuba

DW moja kwa moja kwenye simu yako kupitia WhatsApp

Sasa shabiki wa DW popote pale ulipo unaweza kupokea habari, picha, vidio na sauti zenye ujumbe wa kukuchangamsha moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kupitia huduma ya DW WhatsApp.
Sasa Idhaa ya Kiswahili ya DW inawasiliana nawe moja kwa moja kupitia WhatsApp. Sasa Idhaa ya Kiswahili ya DW inawasiliana nawe moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Huduma hii ni mpya na haina malipo yoyote kupitia mtandao wa WhatsApp. Ni rahisi sana kujiunga na huduma hii. Unachohitaji ni simu yako tu yenye huduma ya intaneti na pia WhatsApp. Baada ya hapo, ingia kwenye #link:http://bit.ly/1Q86kjt:kiungo cha DW Kiswahili WhatsApp# na jaza namba yako na kisha tuma kwa kufuata maelekezo yaliyowekwa hapo.
Baada ya hapo, tutakuweka kwenye orodha ya watu wanaopokea ujumbe kutoka kwetu kila tunapotuma taarifa mpya.
Kuwa mmoja wa marafiki zetu kwenye jamii ya DW WhatsApp, uwe karibu kabisa na habari mpya na ujumbe wa moja kwa moja kwenye simu yako. DW iko nawe popote ulipo.
Mueleze na rafiki yako kwa kumtumia link yetu hiyo. Huduma hii ni ya bure kabisa.

Monday, November 7, 2016

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Samwel Sitta amefariki dunia.

========


4494_b.jpg
Tunasikitika kuwataarifu kuwa mzee wetu mpendwa Samwel Sitta amefariki dunia katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani saa 7:30 kwa muda wa Ujerumani alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume.

0502f3ea-1ffd-4cc2-b748-74e35ff8db86.jpg

Historia yake:

Samuel-Sitta.jpg
Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI.

Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria (L LB) mwaka 1964 na kuhitimu mwaka 1971.

Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka 1966, wakati yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM, wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi ilikuwa na mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa?

Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Mwalimu Julius Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili. Miezi miwili baadaye akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi hao.

Watukutu wawili – Sitta na Wilfred Mwabulambo (Wote sasa marehemu) na wengine kadhaa – waliojitia wazimu na kutetea kile walichokiita haki zao, (haki za wakulima na wafanyakazi), walimshutumu Mwalimu Nyerere kwa maneno makali wakidai “…ni heri wakati wa ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu”.

Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao”. Miezi kumi baadaye, baada ya Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia akaamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392. Viongozi wa mgomo; Sitta na wenzake 7 walitiliwa ngumu, hawakurejeshwa chuoni.

Busara za viongozi wa chuo zilifanya Mwalimu aliliwe zaidi na kuandikiwa barua mbili maalumu na chuo zenye Kumb. Na. C3/Sa.13 ya 2/3/1967 na C3/Ss.13 ya 9/07/1967. Mwalimu alikubali kilio hicho na kuwaruhusu vijana hao wanane warudi kwa sharti kwamba wale watukutu wawili (Sitta na Mwabulambo) watandikwe viboko na “Mwalimu Nyerere” mwenyewe. Hii ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971.

Wakati Sitta anarudi chuoni tayari alikuwa mwajiriwa wa Kampuni ya Mafuta ya “CALTEX OIL” kama Meneja wa Tawi (1967 – 1969) na mwaka 1969 – 1975 aliajiriwa na Shirika la Maendeleo la Taifa kama Katibu na Mkurugenzi wa Utawala.

Baadaye mwaka 1976 Sitta aliamua kujiendeleza kielimu katika masuala ya Usimamizi nchini Uswisi kwenye Chuo Kikuu cha IMEDE ambako alihitimu Stashahada ya Juu ya Usimamizi mwaka huohuo 1976.

Chini ya mfumo wa chama kimoja, Sitta alikuwa kiongozi wa juu wa CCM na serikali akiwa mbunge, mkuu wa mkoa na Waziri katika nyakati tofauti na ameendelea kuwa mbunge na waziri katika mfumo wa vyama vingi.

Sitta alimuoa Margareth Simwanza Sitta

Mbio za ubunge

Enzi za chama kimoja 1975 - 1995 Sitta alikuwa mbunge wa Jimbo la Urambo (kabla halijagawanywa na kuwa Urambo Magharibi na Mashariki) na pia alifanikiwa kuwa waziri kwa nyakati tofauti. Kwa mfano wakati wa kipindi cha mwisho cha Mzee Mwinyi, Sitta alikuwa Waziri za Katiba na Sheria.

Mwaka 1995 Sitta aliingia kwenye mapambano mapya ya siasa za vyama vingi na kwa bahati mbaya akawa mmoja wa vigogo walioangushwa na wabunge wa NCCR. Mshindani wake mkuu alikuwa Msina Jacob Abraham. Msina alishinda kwa kura 10,788 dhidi ya 9,497 za Sitta.

Sitta alirudi tena kwenye jukwaa la siasa mwaka 2005 kwenye uchaguzi mkuu na aliwashinda wapinzani wake wakuu Lumatiliza Yotamu Lubungila wa NCCR na Wilson George Ntakamulenga wa CUF. Sitta alipata kura 28,660 (72.3%) na kurejesha heshima yake jimboni Urambo Mashariki. Kurudi kwa nguvu kulimpa nafasi ya kuwania na kuteuliwa na CCM kugombea uspika wa Bunge la Tanzania na akaliongoza Bunge la Tisa aliloliita bunge la Viwango Na Kasi "Speed and Standards" kwa mafanikio na changamoto nyingi.

Mwaka 2010 Sitta alishiriki tena uchaguzi Urambo Mashariki akawashinda wapinzani wake wakuu Msafiri Abdulrahmani Mtemelwa (CHADEMA) na Zombwe Lotto Edward (CUF) kwa kupata kura 19,947 (70.47%). Baada ya ushindi huo, Sitta alijaribu tena kuwania uspika bila mafanikio; utendaji wake wa kuiuma serikali na wakati mwingine kuipuliza kwenye Bunge la Tisa ulimfanya achukiwe na serikali.

Ilipoonekana ana nguvu akatengenezewa “chui wa karatasi” (mshindani), Andrew Chenge. Chenge naye akachukua fomu ya uspika ghafla, likatengenezwa ‘zengwe’ kuwa wagombea wote wana nguvu, hapo CCM ikapata mwanya wa kutamka kuwa haiwataki wote ili kuondoa mvutano. Sitta akapoteza ndoto za uspika na ukahamia kwa mwanamama Anne Makinda.

Rais Jakaya Kikwete alipotangaza Baraza la Mawaziri mwaka 2010 alimpa Sitta Wizara ya Afrika Mashariki kama Waziri,vilevile alihamishiwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Mbio za urais

Samuel John Sitta alianza mbio za urais “kimyakimya” tangu alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa (2005 – 2010). Kuna nyakati alikuwa akitoa kauli zinazoashiria kuwa nchi inayumba na haina uongozi thabiti huku akionyesha kuwa nchi ina viongozi thabiti na hawajapewa uongozi mkuu wa nchi, akiwemo yeye.

Hata alipoliongoza Bunge la Katiba mwaka 2014, mara nyingi Sitta alionekana kama mtu mwenye shauku kubwa na urais na alipohojiwa, mara kwa mara, juu ya urais alionyesha ana ndoto hizo. Mara kadhaa, alilalamika kuwa wala rushwa wakubwa wanampiga vita kwa sababu ni msafi.

Katika Uchaguzi wa 2015, Sitta alitangaza nia ya kuwania Urais na alichukua fomu ya kugombea urais kupita chama cha Mapinduzi ambapo baada ya uchaguzi wa ndani chama, John Magufuli ndo jina lililofanikiwa kupenya na kuteuliwa na chama kugombea Urais wa Tanzania.

Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amen.

Uchaguzi Marekani: Nani atashinda?

Mfuasi wa Trump


Image copyright AFP

Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika hapo kesho kuchagua atakayemrithi Rais Barack Obama. Je, hali ikoje sasa na nani ana nafasi nzuri ya kushinda?
Mwandishi wa BBC wa Amerika Kaskazini Anthony Zurcher anachambua:
Leo Jumatatu ni siku nyingine ambayo wimbi la uungwaji mkono linatarajiwa kubadilika, hasa baada ya FBI kutangaza kwamba hawajapata ushahidi dhidi ya Bi Hillary Clinton baada ya kuchunguza barua pepe zilizopatikana hivi majuzi.
Bi Clinton anaendelea kuongoza dhidi ya mgombea wa Republican Donald Trump kwenye kura ya maoni ya kitaifa ya Washington Post/ABC, uongozi wake ukiwa alama tano. Kwenye kura ya maoni ya IBD/TPP, Bw Trump anaongoza kwa alama moja.
Hivyo, ni vigumu kubaini hali halisi kutoka kwa kura za maoni.
Aidha, kura zote za maoni ambazo zimefanywa kufikia sasa hazikuzingatia habari za karibuni zaidi za FBI kumuondolewa Bi Clinton makosa.
Lakini kunaweza kukatokea jambo la kuwashangaza watu?
Ukitazama kura za maoni katika majimbo muhimu, kunaonekana kuwa na udhaifu kidogo kwenye ngome ya Clinton.
Hii inaweza kuwa ndiyo sababu Bw Trump anatumia muda mwingi sana kwenye kampeni majimbo ya Michigan, Wisconsin na New Hampshire. Hillary Clinton akiwa Detroit

Image copyright Reuters
New Hampshire, ni moja ya majimbo ambayo yameonekana kuunga mkono chama cha Democratic kwa dhati miezi ya karibuni, lakini sasa jimbo hilo linaonekana kushindaniwa sana. Si ajabu kwamba Bi Clinton na Rais Barack Obama wamepanga mikutano ya dakika za mwisho kuimarisha uungwaji mkono.
Na katika jimbo la Michigan, ambapo Obama alishinda kwa kuwa mbele alama 10 mwaka 2012, mambo hayaonekani kuwa salama sana kwa Democratic.
Lakini kuna habari njema kwa Bi Clinton kutoka Ohio, ambapo utafiti wa maoni uliofanywa na kampuni ya kuaminika unamuonesha akiwa mbele kwa alama moja (hata hivyo, alama hiyo moja bado imo eneo la makosa yanayoweza kutokea kwenye utafiti).
Ikizingatiwa kwamba upigaji kura za mapema unaonyesha watu wengi weusi, ambao ni wengi kiasi eneo hilo, hawajajitokeza sana, Bi Clinton amefika huko siku za karibuni kufanya kampeni.
Alihudhuria tamasha ya muziki ya rapa Jay-Z na nyota wa muziki wa pop Beyonce siku ya Ijumaa kisha akahudhuria hafla ya pamoja na nyota wa mpira wa kikapu LeBron James Jumapili.
Ushindi wa Clinton Ohio unaweza kuimarisha sana nafasi yake kushinda, kwa hivyo ishara za matumaini - baada ya kura kadha za maoni awali kuonyesha alikuwa nyuma ya Trump - ni habari njema.
Bi Clinton atafurahia hali jimbo la Nevada, ambapo kumekuwepo na foleni ndefu za wapiga kura wa mapema, ishara kwamba watu wa asili ya Hispania (Latino/Mexico) wamejitokeza kwa wingi.
Kwa jumla, ana nafasi nzuri ya kushinda ukimlinganisha na mpinzani wake lakini lolote linaweza kutokea.Clinton na Trump

Image copyright AFP
Kwa mujibu wa:
  • New York Times Upshot: Clinton ana uwezekano wa 84% kushinda
  • FiveThirtyEight: Clinton ana uwezekano wa 65% kushinda
  • HuffPost: Clinton ana uwezekano wa 98% kushinda