Wednesday, December 28, 2016
Wednesday, November 9, 2016
Tuesday, November 8, 2016
Anayemkataa
Magufuli anawakumbatia mafisadi
Na Adelinus Banenwa
“Siku za mwizi ni
arobaini” haya ni maneno ya wahenga ambayo hayana kipingamizi kwa hali ya sasa inayoendelea
nchini Tanzania baada ya siku takribani therathini na tano tangu tumpate raisi
mpya wa awamu ya tano ambaye aliapishwa November 5 mwaka huu na kukabidhiwa
nchi kutoka kwa mtangulizi wake
Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli anaendelea kuonekana wa
tofauti kutokana na kasi yake ya utendaji japo walio wengi hawashtushwi na kasi
yake hiyo kutokana na kujulikana vyema hata wakati akiwa waziri katika wizara
mbalimbali kama vile wizara ya ardhi, uvuvi, pamoja na na wizara ya ujenzi
Anajulikana kuwa mtu mwenye misimamo isiyo teteleka,
anaichukia rushwa, hana makundi kwenye chama chake, hawakumbatii mafisadi, haya
yote yanamfanya aendelee kuwa maarufu na kuzidi kupendwa na watanzania
waliokata taama na nchi yao kwa muda mrefu
Katika kampeini zake tangu alipoteuliwa na Chama Cha
Mapinduzi CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya uraisi
alikuja na kauli mbiu inayosema “hapa
kazi tu” wengi wa wananchi walisema kauli hii inaakisi utendaji wake wa
kazi katika chakato wa kuomba lidhaa kwa
wananchi wamchague ili awe rais wa awamu ya tano aliweza kutembea kwa barabara
zaidi ya kirometa elfu arobaini huku akisisitiza kuwa mabadiriko yanawezekana
ndani ya CCM
Uchaguzi uliyokuwa na ushindani usiyo kuwa wa kawaida na ambao haukuwai kutokea
katika historia ya Tanzania tangu ilidhie mfumo wa vyama vingi 1992 na uchaguzi
wa kwanza mwaka 1995kwa kuwa hadi siku ya kupiga kura hakujulikana nani
atashinda licha ya kuwa “mwamba ngoma uvutia kwake” pengine kutokana na
umaarufu wa wagombea hasa kutoka vyama vikuu nchini Chama Cha Mapinduzi CCM
kikiwakirishwa na Magufuli na Chama cha Demokrasia
na Maendelea CHADEMA kikiwakilishwa na Edward Lowassa
Tarehe 29 october mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Tanzania
jaji mstaafu Damiani Lubuva alimtangaza mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM
John Magufuli kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa asilimia 58.46% na kuaapishwa
tarehe 5 november kwa kutekeleza kauli
yake ya hapa kazi tu rais Magufuli alianza kazi siku ya pili yake baada ya
kuapishwa yaani tarehe 6 kwa kufanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha na
kukuta takribani wafanyakazi sita hawapo ofisini wakati ni muda wa kazi
Magufuli hakuishia hapo alifanya ziara nyingine ya kushtukiza
hospitari ya rufaa ya Muhimbili na
kukuta hali mbaya kwa wagonjwa pamoja na vifaa tiba huku mashine city scan
zikiwa hazifanyi kazi kwa zaidi ya mwezi
mmoja. maamuzi ya kuvunja bodi ya muimbili na kumsimamisha
kazi mkurugenzi wa hospitali hiyo ilikuwa hatua ya mwanzo katika kuhakikisha
utekelezaji wa kauli mbiu yake na kutoa wiki mbili mashine hizo ziwe zinafanya
kazi
Ziara za kushtukiza kwa kiongozi huyo hazikuishia hapo,baada
ya hapo aliamia bandari na kuibua wizi uliokuwa ukiendelea bandarini hapo ikiwa
ni pamoja na upotevu wa makontena, ukwepaji wa kulipa kodi uliokuwa ukifanywa
na wafanywa na biashara wakubwa jambo lilimpelekea Rais kumsimamisha kazi mkurugenzi
wa bandari kabla ya kuvunja bodi ya
bandari hiyona kulitaka jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa wote kwa ajili
ya uchunguzi.
Hatua ya kupunguza matumizi ya serikali na kuelekeza nguvu
zake katika kuinua uchumi wa taifa Rais Magufuli ameamua kufutilia mbali baadhi
ya sherehe zilizokuwa zimezoeleka kuadhimishwa kwa shamra shamra ndermo na
vifijo kama sikukuu ya uhuru , siku ya ukimwi na badala yake fedha hizo
zitumike katika kununulia madawa pamoja na vitanda vya hospitali ya rufaa ya
Muhimbili na kupanga siku hizo kufanyika usafi wa mazingira nchi nzima
“hatuwezi kuadhimisha miaka 54 ya uhuru huku watu wanakufa kwa kipindupindu”
alisema Rais Magufuli
Mpaka sasa Rais Magufuli anaendesha nchi akiwa na Waziri mkuu
Kassim Majaliwa ambaye pia kasi yake ya utendaji imeonekana kuwa sambamba na
Magufuli mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika shirika la reli
Tanzania na Zambia (TAZARA) na kugundua madudu ya ubadhirifu wa fedha uliokuwa
ukiendelea katika shirika hilo
“Anayemkataa Magufuli anawakumbatia mafisadi” alisema
kiongozi wa chama cha ACT Wazarendo Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni mbunge wa
Kigoma mjini kupitia chama hicho alitoa kauli hiyo mnamo November 22 mwaka huu
huku akiwataka wananchi kumuunga mkono katika kupambana na ufisadi uliokithiri
hapa nchini hasa katika sekta za umma
“Nilipokuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge nilikuwa nikitoa
taarifa mbalimbali zinazohusu wizi na uporaji uliofanywa katika ubinafsishwaji,
sasa tumepata Rais anayetaka kupambana na ufisadi na kurudisha viwanda hivyo
tunapaswa kumuunga mkono”alisema Zitto
Rais Magufuli amevunja rekodi ya watangulizi wake kwa
kuendesha nchi zaidi ya siku 30 bila kuwa na baraza la Mawaziri ambapo anafanya
kazi na Waziri mkuu pamoja na Makatibu wakuu wa wizara husika huku utendaji ukionekana kuwa wa kasi
ya ajabu licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa zikiwemo za kuwamaliza mafisadi
na wala rushwa katika ofisi zote za umma na kudhibiti mianya waliokuwa
wakitumia.
Kama alivyofanikiwa kudhibiti safari za nje kwa viongozi na
kuzuia viongozi hao kutotumia viti vya daraja la kwanza ndani ya ndege,na
kuzuia manunuzi ya magari mapya ya serikali kwa lengo la kupunguza matumizi ya
serikali na kuongeza pato la Taifa.
Utendaji kazi wa Magufuli umesababisha mgogoro mkubwa wa
Afrika Mashariki ambapo wananchi kutoka Kenya wamemtaka Rais wao Uhuru Kenyata
aige mfano wa Rais wa Tanzania katika kuibua na kudhibiti ufisadi uliokithiri
nchini Kenya, vivyo hivyo hata nchini Uganda.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mapema wiki hii ametakiwa na
wananchi wake kuiga mfano wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi na kudhibiti
rushwa pamoja na mfumuko wa bei nchini Nigeria wakati wakizungumza na shirika
la utangazaji BBC
Kauli ya Zitto kuwa anayemkataa Magufuli anawakumbatia
mafisadi haina kipingamizi kwani mambo yaliyoshindikana kwa miaka mingi
yameweza kufanikishwa ndani ya muda mfupi, ni vyema wananchi wakampa
ushirikiano katika safari hii aliyoianzisha
Subscribe to:
Posts (Atom)