
Rais Vladmir Putin wa Urusi amebeza uvumi kuhusu afya yake katika siku yake ya kwanza kuonekana hadharani baada ya siku kumi.
Kiongozi
huyo wa Urusi amesema"maisha yangekuwa ya kuchosha iwapo kusingekuwa na
umbeya", lakini ameshindwa kueleza kuhusu kutoonekana kwake hadharani
kwa kipindi hicho na kufuta ratiba iliyomtaka kuhudhuria matukio kadha
aliyokuwa amepangiwa.
Alionekana katika mkutano na rais mwenzake
wa Krygyzstan Almazbek Atambayev katika kasri ya Constantine karibu na
mji wa St Petersburg.
Bwana Putin Jumatatu alitoa amri kwa askari
karibu elfu arobaini wa jeshi la wanawamaji wa Urusi kujiandaa kwa
mazoezi ya kivita, hatua ambayo huenda ikawa ni kujibu mazoezi ya
majeshi ya NATO yaliyofanyika karibu na nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment