Friday, September 25, 2015

Kafando arejea rasmi madarakani Burkina Faso

Rais Michel Kafando wa Burkina Faso aliyekuwa amepinduliwa kwa wiki moja amerejea rasmi madarakani huku Umoja wa Ulaya ukisema ni hatua muhimu ya kulirejesha taifa hilo kwenye utawala kamili wa kiraia.
Rais wa serikali ya mpito ya Burkina Faso, Michel Kafando. Rais wa serikali ya mpito ya Burkina Faso, Michel Kafando.
Huku mitaa ya mji mkuu, Ougadougou, ikitandwa na nderemo na vifijo na vijana wakiimba wimbo wa taifa, Rais Michel Kafando alirejea rasmi kwenye ikulu jioni ya jana, wiki moja kamili baada ya jenerali mmoja wa kijeshi na wafuasi wake kumuondoa madarakani na serikali yake ya mpito.
Hata hivyo, sherehe rasmi za kurejea madarakani kwa Kafando na Waziri Mkuu Yacoub Isaac Zida zilifanyika bila kuhudhuriwa na kiongozi wa jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa, Jenerali Gilbert Diendere, ambaye alilazimika kusaini makubaliano ya kuachia madaraka baada ya jeshi tiifu kwa serikali kumpa muda wa masaa 48 kufanya hivyo, ama vyenginevyo kukabiliwa na hatua kali.
Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Kafando aliwashukuru wananchi na jumuiya ya kimataifa kwa kumuunga mkono muda wote. "Kusingekuwa na namna nyengine zaidi ya hii kufuatia kilio cha umma dhidi ya watenda uovu na lawama za kimataifa dhidi ya waliojichukulia madaraka kwa nguvu, na japokuwa serikali yangu ya mpito yenyewe haikuwa imechaguliwa kwenye uchaguzi huru, muliiamini na bado ndicho chombo pekee kinachowakilisha matakwa ya umma wa taifa hili," alisema Kafando.
Muda mchache baada ya Rais Kafando kuhutubia taifa, kiongozi wa mapinduzi hayo yaliyoshindwa, Jenerali Diendere aliliambia shirika la habari la AFP kwamba kitendo chao kilikuwa kosa lililokosa uungwaji mkono wa umma.
Vijana wakipinga utawala wa kijeshi uliongia madarakani kwa nguvu mjini Ougadougou. Vijana wakipinga utawala wa kijeshi uliongia madarakani kwa nguvu mjini Ougadougou.
"Mapinduzi yamekwisha. Kufanya mapinduzi haya lilikuwa kosa kubwa kuliko yote. Tumejuwa kuwa umma haukuyataka. Na ndio maana tumeondoka," alisema mkuu huyo wa zamani wa ujasusi kwenye serikali ya Rais Blaise Compaore.
Rais Compaore mwenyewe alilazimika kuikimbia nchi mwezi Oktoba mwaka jana, baada ya kukabiliwa na maandamano ya umma.
Ushindi wa ECOWAS
Kushindwa kwa mapinduzi hayo na kurejea madarakani kwa Rais Kafando kunatokana kwa kiasi kikubwa na juhudi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo ilianzisha haraka mchakato wa kurejesha utawala wa kiraia mara tu baada ya mapinduzi kutangazwa.
Umoja wa Ulaya, ambao ulikuwa umeungana na jumuiya ya kimataifa kuyalaani mapinduzi hayo, umeikaribisha hatua ya kurejea madarakani kwa Kafando. Taarifa iliyotolewa na Umoja huo kutokea Brussels, inasema kurejea kwa Kafando kunasawazisha hali ya mambo nchini Burkina Faso, wakati taifa hilo likielekea kwenye utawala kamili wa kiraia.
Kabla ya mapinduzi hayo, uchaguzi mkuu ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 11 Oktoba, lakini sasa Waziri Mkuu Isaac Zida amesema uchaguzi huo umesogezwa mbele kwa wiki kadhaa kutokana na sababu za kiufundi.
NA K-VIS MEDIA 
CELINA Ompeshi Kombani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Utumishi), amefariki dunia akiwa kwenye matibabu nchini India. Kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, Marehemu Kombani alipelekwa nchini India mwezi mmoja uliopita akisumbuliwa na malaria iliyoambatana na homa kali.
Kwa mjujibu wa Ndugai, Mh. Kombani ambaye mara ya mwisho alikuwa mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki, amefariki jioni hii ya Septemba 24, 2015 na mwili wake utawasili jijini Dar es Salaam, Jumamosi Septemba 26, 2015.
Mh. Kombani aliyezaliwa 19 June 1959,
alipata elimu yake ya msingi Kwiro kuanzia mwaka 1968 hadi 1975, na baadaye kujiunga na shule ya sekondari Kilakala mwaka 1975 hadi 1978. Mnamo mwaka 1979 alijiunga na shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora, (Tabora Girls), na kuhitimu mwaka 1981.

Mwaka 1982, Mh. Kombani alijiunga na Chuo cha IDM Mzumbe na kujipatia shahada ya Utawala wa Umma (B.A in Public Administration mnamo mwaka 1982 hadi 1985. Mwaka 1994 hadi mwaka 1995 Mh. Kombani alichukua shahada ya pili ya Utawala wa Umma, chuo Kikuu ch Mzumbe

Msiba baada ya mamia kuuwawa Mina

Zaidi ya mahujaj 700 wameuwawa na mamia kujeruhiwa kufuatia vurumai na mkanyagano huko Mina.Huo ni msiba mmojawapo mkubwa kabisa kutokea wakati waumini wa dini ya kiislam wanapotekeleza nguzo ya tano ya dini yao.
Waumini wakifanya ibada Karibu na mlima Arafat nje ya Macca
Ni msiba mkubwa kabisa kuwahi kugubika Hijja tangu miaka 25 iliyopita.Mahujaj zaidi ya milioni mbili wamekusanyika mwaka huu.
Mfalme Salman aliyekutana na wakuu wa maandalizi ya Hajj amesema anasubiri haraka matokeo ya uchunguzi,na kuongeza ameamuru mipango ya maandalizi ya Hijja idurusiwe ili kuhakikisha waumini wanatekeleza salama kabisa wajib wao kuambatana na nguzo ya tano ya dini ya kiislam.
"Bila ya kutilia maanani matokeo ya uchunguzi,juhudi za kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa Hajj hazitosita.Tumezitaka taasisi husika zidurusu sera zao na jinsi ya kutoa dhamana."Amesema mfalme huyo.
Akizungumzia hapo awali kuhusu ajali hiyo,waziri wa afya wa Saud Arabia Khaled al Faleh aliwalaumu kwanza mahujaj kwa kile alichokitaja kuwa "kutotilia maani muongozo..Lakini msemaji wa wizara ya mambo ya ndani,jenerali Mansur Turki alionekana kuwa na tahadhari zaidi aliposhauri watu wasiharakishe kusema kitu kabla ya matokeo ya uchunguzi kutangazwa.Amesema tu "joto kali na kuchoka sana mahujaj vimechangia kuifanya idadi ya wahanga iwe kubwa mno.
Walimwengu waelezea huzuni zao
Wauguzi wakiwahudumia majeruhi wa Mkaganyagano wa Mina
Wakati huo huo walimwengu wanaomboleza.Ikulu ya Marekani,katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon,serikali kuu ya Ujerumani,Ufaransa,mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Ulaya,Donald Tusk na Uturuki wametuma rambi rambi zao kutokana na msiba huo.
Katika wakati ambapo wengi wa mahujaj ni wageni,Iran imesema mahujaj wake wasiopungua 131 wamefariki kufuatia ajali hiyo.Kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei amewatwika jukumu la ajali hiyo viongozi wa Saud Arabia na kukosoa "usimamizi mbaya."
Usimamizi wa Hija wakosolewa
Mahujaj wanaendelea kumtupia mawe shetani
Lawama kama hizo zinatolewa pia na mahujaj wanaosema wanaogopa kuendelea kuhiji.Mohammed Hassaan,raia wa Misri mwenye umri wa miaka 39,anasema anaogopa kuendelea kuhiji,isije ikatokea ajalai nyengine ya msukumano leo hii,akitaja pia usimamizi mbaya wa pirika pirika za mahujaj zaidi ya milioni mbili waliokusanyika Mina,kilomita chache kutoka Macca.
"Saud Arabia inatumia fedha nyingi kwaajili ya Hijja,lakini maandalizi yana kasoro"amesema hujaj mwengine,Ahmed wa kutoka Misri.
Licha ya hofu lakini,waumini waliodhamiria kukamailisha nguzo ya tano ya dini ya kiislam,wanaendelea hii leo kumtupia mawe shetani.
Hujaj mmoja wa kutoka Syria anasema anaendelea na Hijja kwasababu tunanuku " Mungu anawalinda."

Sunday, September 6, 2015


RAIS WANGU KIKWETE UONGOZI WETU KAMA KISHADA TUTOKAKO TUENDAKO HAKUJULIKANI!
Na Adelinus .D. Banenwa;.
Rais wangu moja kati ya sifa nyingi za mtu dhaifu ni uoga. Anaogopa hata kivuli chake. Serikali ya Awamu ya nne ikisikia kuna mgomo au hasa maandamano, inatetemeeeka, utadhani ni utete dhaifu unaosukumwa na mkondo mkali wa maji ya mto yaendayo kasi! Yohani, ‘John Pombe Magufuli’ ni uzao halisi wa udongo wa nchi hii. Amefukua vya kufukua!
Katumbua jibu na sasa usaha unamwagika. Mwenye jipu yaani serikali, inanuka usaha mwili mzima! Kwakuwa Wahenga wenye busara walisema dawa ya jipu ni kulitumbua na kwakuwa Waziri wetu wa Ujenzi amelitumbua, basi wote wenye mapenzi mema wanapaswa kumpongeza kwa kazi njema aliyoifanya.
Rais wangu palipo na ukweli tutasema. Lazima tuusimamie ukweli hata kama kwa kuusema ukweli huo mjinga atasema tunamchukia mtu na mpumbavu atasema tumenunuliwa na mtu! Kuacha kusema ukweli kwa kuogopa kuonekana unamchukia mtu au kuogopa kusemwa umenunuliwa ni upungufu alionao mwanadamu dhaifu. Jasiri hatikiswi na hilo!
Magufuli sifahamiani naye, lakini ni mtu mwema gani asiyeujua utendaji kazi wake ulivyo mahiri? Tangu waende akina Sokoine na Mrema nani mwingine wakutolea mfano?
Huyu siyo malaika. Aliposhirikiana na genge la walanguzi tukulangua nyumba zetu, wenyewe wakiziita za serikali tulimlaani wote! Na kwa hilo hajasamehewa! Na hatasamehewa mpaka pale atakapowarudishia wananchi nyumba zao! Lakini kwakuwa hatuko hapa kuangalia sura za watu, tuko hapa kujadili utendaji kazi mahiri kwa maslahi ya nchi yetu na wananchi wake, anayefanya jambo jema kama alilolifanya Magufuli, kusimamia sheria za nchi, hatuna budi tumpongeze wote.
Kiongozi wa haki mwenye ufahamu timamu akiambiwa ukweli hata kama utamuumiza, atamheshimu aliyemwambia huo ukweli, akijua kuwa huyo ndiye aliye na mapenzi ya kweli naye. Na ikimpendeza atamtumia!
Rais wangu wapinzani wanapokwambia waondoe mawaziri wanaokupotosha hawamchukii mtu wala hawawachukii hao mawaziri! Wanakutakia mema Rais wangu! Hawataki uonekane wa ajabu mbele ya watu wako! Tunaoishi na wananchi huku mitaani, vijijini na mashambani tunaambiwa mengi. Ningekuwa na faragha na wewe mengine ningekuwa nakunong’oneza, ili ukinieleza niwaeleze wapate kukuelewa kwa maana wako wanaokupenda! Kwa kuwa sina faragha na wewe nakuwekea maneno ya wananchi wako hapa ili ukiyasoma ujue ni picha gani wanaokuzunguka wanakutengenezea mbele ya wananchi!
Mwanamwema kutoka Iringa aliniandikia ujumbe ambao na mimi nauweka hapa vilevile alivyoandika! Aliandika, “Mwalimu nimesikitishwa sana na hotuba ya rais iliyoangaliwa hata na watoto wadogo. Hivi kwa nini anamshambulia mwananchi wake kwa maneno makali kama yale? Halafu kwa nini kila kitu anasema ‘nimeambiwa’? Falsafa yake ya mbayuwayu imemshinda? Sasa tena tunaambiwa kumbe hata mswada wenyewe hajausoma. Kazi tunayo. Nchi za kiafrika haziendelei na moja ya sababu ni kuongozwa na watu wenye kuambiwa.”
Rais wangu usipokuwa na pupa utaona kuwa watu wako wanakujali lakini unawakatisha tamaa! Dunia na Ulimwengu vinatambua hivyo! World Happiness Report 2013 iliyoandaliwa na kundi la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa imedai kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa Duniani!
Ndugu Rais yaliyojiri katika sakata la wenye malori na serikali limezidi kuwakatisha tamaa Watanzania. Iliandikwa, ‘Pinda amuonya Magufuli’, wengine wakaandika, ‘Serikali yamzima Magufuli’. Wananchi wakabaki kuulizana, hivi Pinda na Magufuli wako serikali mbili tofauti? Ni serikali gani hii yenye viongozi wenye kauli tofautitofauti? Hawakutani kwenye Baraza la mawaziri kuweka msimamo wa serikali?
Waliosema serikali inapasuka mwanzoni sikuwaelewa. Utoto siyo uchache wa miaka ya kuzaliwa peke yake! Wala kufanya upuuzi siyo lazima umtukane mtu. Kwakuwa hawa ni waheshimiwa huwezi kuweka neno watoto au wapuuzi. Isipokuwa viongozi wa serikali moja kuonekana mbele ya wananchi kama wanatunishiana misuli, ni vyote viwili, utoto na upuuzi!
Rais wangu Magufuli anasema anazilinda barabara zetu zisife haraka! Mpaka hapa kuna ubaya gani? Je, mamlaka hayo anayo? Kaonyesha sheria iliyotungwa na Bunge kihalali kabisa! Kumbe mamlaka anayo kufuatana na sheria! Sasa ndugu Rais huyu anayemzima Magufuli au kumuonya yeye alisomea wapi?
Kwa mdomo wake Waziri Mkuu wetu anasema, “Hatua zilizochukuliwa na Dk Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria. Tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamzi wa pamoja”. Jamani sheria ikishatungwa mnashauriana nini tena?
Akaongeza, “Sasa suala la asilimia tano, lilitokana na ombi la wadau wa usafirishaji kwa aliyekuwa waziri wa Ujenzi miaka ya nyuma na haikuwa sheria kamili. Limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya.” Kudai kwa nguvu wakati huna sheria nikufanya fujo!
Bado anakiri kuwa limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya! Yaani wenye malori walitumia vibaya ombi lao. Magufuli kuona hivyo amelifuta. Kwa maelezo haya ya Waziri mkuu Magufuli amekosea wapi? Kama ombi hilo ovu liliridhiwa na Waziri wa Ujenzi wa miaka ya nyuma kwa maslahi ya nchi au kwa maslahi ya wenye malori na waziri mwenyewe haijulikani. Kinachojulikana ni kwamba waziri huyo hivi sasa serikali imemfikisha mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa ofisini siku hizohizo za nyuma.
Waziri mkuu anasema kosa la Magufuli ni kuilinda hiyo sheria bila kuwashirikisha wanaoivunja. Jamani, unapomkamata mwizi unamshirikishaje? Unashauriana naye nini ili mpate uamuzi wa pamoja kama siyo kutaka kumwomba rushwa?
Mzee Peter Kisumo anasema, “Chama kimebaki cha walalamikaji, kila mtu amekuwa mlalamikaji. Hata Waziri mkuu amegeuka mlalamikaji. Sijaona watu wanaowajibishwa kwa ufisadi!”
Rais wangu bado Waziri mkuu bila sababu ya msingi anaunda tume sijui kamati ambayo hata hivyo haina uwezo wa kuifuta wala kuirekebisha sheria hiyo! Huku ni kufuja kodi ya wananchi? Ndugu Rais ni hivi majuzi tu wananchi kwa huzuni kubwa wameshuhudia mwandishi wa habari Ufoo Saro, baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi kadhaa wanawema walimkimbiza hadi Hospitali ya Serikali ya Tumbi lakini akakosa huduma ya matibabu kwasababu Hospitali hiyo haikuwa na mashine ya Xray.  Kwanini fedha zitakazotumika na tume hii na tume nyingine za aina hii zisingetumika kununulia mashine ya Xray kwa Hospitali hii? Umuhimu wa Hospitali ya tumbi uko wazi. Inapokea majeruhi kila siku watokanao na ajali za mara kwa mara zitokeazo katika barabara hii katili ya Morogoro! Mungu huyu! Maisha ya wananchi hayana maana mbele ya wenye malori!
 Serikali inayojiendesha bila kutegemea ufadhili wa wafanyabiashara hasa wakati wa kampeni, wenye malori wangepata wapi kiburi cha kugoma? Sheria kama haifai hurudishwa Bungeni ikafutwe au ikarekebishwe huku kazi zikiendelea! Wakati wa Uwaziri mkuu wa Sokoine au wakati wa Mrema, mwenye lori gani angethubutu kuinua pua yake juu? Serikali kuruhusu kikundi fulani cha watu, wawe wenye malori au wenye asili fulani, waendelee kuvunja sheria halali huku wananchi wengine wakiona ni mfano halisi wa uongozi mbovu! Bila kufahamu serikali inawasukuma na wengine wavunje sheria zinazowakera. Chanzo cha maandamano na migomo isiyokwisha ni uongozi mbovu!
Ndugu wananchi kitabu cha mwalimu mkuu wa watu kinaelekeza wazi kuwa jiandaeni kupokea fedha zitakazochangwa na hawa jamaa. Mkiletewa wakati wa kampeni zichueni, lakini kura msiwape! Kuita wenye malori ili muafikiane wakati sheria iko wazi ni kielelezo cha uongozi ulioshindwa kuongoza! Yanini Kuwa na kiongozi wa namna hiyo? Tumeliona hili kwenye tozo ya simu. Baada ya kusikia kelele za wananchi ikaamriwa mawaziri na wamiliki wa kampuni za simu au wadau wakae pamoja wafikie muafaka. Kiko wapi! Uongozi ulioshindwa!
Rais wangu uongozi wa nchi unapokuwa laini kiasi hiki, wananchi wanapoletewa habari za kutisha kuwa magaidi wameshamiri nchini mwetu matumaini yao wayaelekeze wapi? Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, linawashikilia vijana 11 kwa tuhuma za kukutwa mafichoni katika msitu wa mlima Makolionga wilayani Nanyumbu wakifanya mazoezi ya kijeshi. CD walizokutwa nazo ni za kundi la kigaidi la Al Shabaab. Zinaonyesha watu wakichinjwa, mauaji ya kiongozi wa Al Qaeda Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, kuaandaa majeshi, mauaji ya Idd Amin na Mogadishu Sniper.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara Zellote Stephen anasema watuhumiwa walikamatwa, baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema. Wananchi wanauliza bila wasamaria wema magaidi hao si wangemaliza mafunzo yao halafu wakaenda kwenye utekelezaji bila polisi kuwa na habari? Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi?
Katikati ya habari hizo zinakuja habari nyingine zinazoarifu kuwa, Ramadhani Twaha mkazi wa mtaa wa Kirumba jijini Mwanza amefikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Mara. Anatuhumiwa kukutwa akisambaza CD zenye machapisho ya kigaidi katika msikiti wa Ibadhi ulioko mjini Bunda ambazo zina mafunzo ya kijeshi na zinazochochea vurugu. Matukio haya mawili yanaashiria jinsi mtandao wa kigaidi ulivyosambaa nchini. Zinaingizwa vipi na kusambazwa vipi nchini? Nani wanaingiza CD hizi? Usalama wetu ni wa mashaka matupu!
Mafunzo  katika msitu wa Makalionga yalifanywa kwa muda gani? Je, kundi hilo la watu 11 lilikuwa ni kundi la ngapi? Ni katika msitu wa Makalionga tu ndiyo mafunzo hayo yanakofanyika? Je, waliyokuwa wanapewa mafunzo waliambiwa malengo ya mafunzo hayo? Walimu wao wako wangapi na wako wapi? Wanafadhiliwa na nani? Je, huu siyo mwanzo wa vita vya msituni?
Ndugu Rais raia kutoa taarifa kama hiyo kwa jeshi la polisi ni muhimu na ni ishara ya uzalendo kwa nchi yake, lakini huko kuwe ni kusaidia tu! Hilo ni jukumu la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kugundua vyenyewe hatari zinazolinyemelea Taifa letu! Liwalo na liwe, wenye malori tu hivi! Magaidi mtawaweza vipi?
Rais wangu tunaacha ya kwetu tunadandia ya wengine. Viongozi wako kimbelembele kusaka sifa za bei poa. Nchi yetu ilipopata nafasi adhimu ya kulihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa baadhi ya wananchi walisikika wakiusikitikia muda ambao kwa maoni yao uliotumika vibaya kuisema ICC badala ya kuyapa nafasi matatizo lukuki yanayoisibu nchi yetu! Nchi yetu ina ugomvi gani na ICC?
Rais wangu ni uzalendo kwa bara la Afrika na Waafrika wenzetu ndiyo vinatusumbua? Hapana! Ni mihemko ya moyo kwa kujihisi tuko kwenye foleni ya kwenda huko kutokana na tunayoyatenda nchini mwetu? Hili linawezekana! Kwanza ziliisha sikika habari kuwa kuna baadhi ya matukio ya kinyama yaliyotokea nchi mwetu ambayo taarifa zake zinatumwa huko! Kujitoa ICC hakuwezi kuzuia tusihukumiwe na mahakama nyingine. Kinachoweza kuzuia tusihukumiwe ni kutotenda unyama dhidi ya raia wetu, kama tunaona tunatenda.
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bwana Koffie Annan amesema ‘itakuwa ni alama ya aibu’ kwa bara la Afrika iwapo litajiondoa katika mkataba wa Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC. Amesema ikiwa viongozi wa Afrika wataipinga na kuipiga vita ICC na kujiondoa, itakuwa ni fedheha kubwa kwa kila mmoja wao na nchi zao. Tumwombee kwa Mungu Rais wangu asije akawa mmoja wao kati ya marais wanaotaka kuziletea nchi zao fedheha hii kubwa! Mwenye fikra ya kulipeleka wazo hili Bungeni huyo ni mufilisi, hafai kuwa kiongozi wetu! Tuna akili gani kubwa ya kutaka kuunga mkono kujitoa ICC kuliko akili ya viongozi waliotutangulia, waliosaini mkataba wa Roma wa kujiunga na ICC?
Bwana Annan amewashutumu viongozi wa Afrika kwa kulinda maslahi yao binafsi na si kwa Waafrika wote huku akisisitiza kuwa njama za nchi za Afrika kutaka kujiondoa ICC ni ishara dhahiri kuwa kuna desturi ya kutoheshimu sheria.
Watuhumiwa wanaokabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo wamefikishwa kama watu binafsi na si kama Bara la Afrika, hivyo dhana kuwa ICC ina dhamira ya kuwaandama viongozi wa Kiafrika siyo sahihi!
Mtu mzima tena bila aibu anasema kati ya walioshitakiwa 30 waafrika ni 27. Hawa ndiyo wale ambao akishtakiwa mhalifu, kama dini yao ni moja anasema wa dini yetu tunaonewa! Kiongozi kuishiwa fikra ni hatari sana. Muhimu hapa ni kujua je, walioshtakiwa ni wahalifu? Muhimu siyo rangi ya ngozi yao.
Mwanamwema Jaji mpya wa Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) Dk Steven Bwana amesema viongozi wa nchi za Afrika wanaotaka kujiondoa kwenye mahakama hiyo, wana lengo la kuficha uovu uliopo katika nchi zao kwani baadhi yao wanajifanya miungu watu!
Amesema, “Afrika kuna viongozi wazuri, lakini tusifiche ukweli wapo waovu, wengine nusu miungu wanaopenda kila kitu kiwe chao, hili halikubaliki. Nchi za kiafrika kujitoa ni aibu, sababu zilizotufanya tujiunge zipo, tunataka kujiondoa kwasababu tunadhani ICC inatufuatilia tunapofanya makosa, ICC inatimiza wajibu, haiwadhalilishi viongozi wa Afrika, watafika kote.”