Sayari inayofanana zaidi na Dunia yagunduliwa
Chombo cha Kepler (nilichokiandkia makala hapo nyuma) kimegundua sayari nyingine tatu ambazo zaweza kumudu maisha. Na moja kati ya hizo tatu, inafanana na Dunia zaidi kuliko Sayari nyingine yoyote iliyogunduliwa hapo nyuma.Sayari hii iliyopewa jina “Kepler-62f” ni sayari yenye miamba, na inazidi ukubwa Dunia yetu mara 1.4.
Sayari hizi zinazunguka nyota moja ambayo ni ndogo na ukilinganisha na jua letu, vile vile mwanga wake ni hafifu kidogo ukilinganisha na jua letu.
Sayari nyingine inaitwa “Kepler-62-e” na inaizidi ukubwa Dunia yetu mara 1.6.
Sayari zote hizi mbili zinazunguka katika “habitabe zone” ya nyota yao (eneo kutoka kwenye nyota ambalo linaiwezesha Sayari kuwa na maji-kiowevu (liquid water)).
Kepler-62e na f ipo miongoni mwa mifumo mipya ya Sayari (planetary systems) iliyogunduliwa hivi karibuni, na ni sehemu nzuri ya kwenda kuchunguza kama kuna namna yoyote ya maisha au viumbe vinavyopatikana huko.
Sayari ya tatu inaitwa “Kepler-69c” na inaizidi Dunia yetu ukubwa mara 1.7, na inaizunguka nyota moja ambayo inafanana kwa karibu na jua letu…
Yote haya ni katika jitihada za kuendelea kutafuta Sayari zinazofana na Dunia, na ambazo zaweza kumudu maisha…
No comments:
Post a Comment